TAASISI ZA ARKUU

Muundo una vitengo sita (6) vilivyo chini ya Afisa Mdhamini vitengo hivyo ni kama vifuatavyo: –

1 – Kitengo cha Uhasibu:

Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya utayarishaji na ufanyaji malipo mbali mbali ndani ya Afisi ya Rais – Kazi Uchumi na Uwekezaji.

2 – Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani:

Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya ushauri na udhibiti wa mali na fedha za Afisi, Kufanya ukaguzi wa matumizi ya rasilimali za Afisi.

3 – Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma:

Kitengo hiki kitahusika na kutoa huduma za ununuzi na na usimamizi wa uondoshaji wa mali za umma ndani ya Afisi.

4 – Kitengo cha Uhusiano:

Kitengo hiki kitahusika na masuala ya mahusiano kati ya Afisi na taasisi nyengine, kuratibu malalamiko na kuzitangaza shughuli za Afisi.

5 – Kitengo cha Sheria:

Kitengo hiki kitahusika na kutoa huduma za ushauri wa masuala ya kisheria katika Afisi ya Rais – Kazi Uchumi na Uwekezaji.

6 – Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano:

Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya kutoa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano ndani Afisi ya Rais – Kazi Uchumi na Uwekezaji