Malengo
Malengo
Afisi Ya Rais Kazi Uchumi Na Uwekezaji ilijiwekea malengo yafuatayo:-
- Kukuza na Kusimamia Uwekezaji kwa Maendeleo ya Nchi
- Kubuni fursa za ajira nchini na kusimamia upatikanaji wa ajira za staha hasa katika Sekta Binafsi
- Kusimamia utekelezaji wa Mikataba ,Sharia na Kanuni za Kazi za kitaifa , Kikanda Na Kimataifa na kuimarisha mahusianio mazuri ya kazi miongoni mwa Serikali,Sekta Binafsi,Waajiri na Vyama vya Wafanyakazi
- Kuimarisha Usalama na Afya kazini
- Kukuza na kusimamia Maendeleo ya Vyama vya Ushirika
- Kukuza na kuimarisha mashirikiano baina ya Sekta Ya Umma Na Sekta binafsi
- Kuratibu uandaaji na utekelezaji wa Sera ,Sharia ,Program Na Tafiti zinazohusiana na masuala ya Kazi ,Ajira ,Uwekezaji,Mashirikiano Baina Ya Sekta ya Umma Na Sekta Binafsi Na Uwezeshaji
- Kuimarisha uratibu,mashirikiano,ufatiliaji na tathmini ya shughuliza Afisi pamoja na kuelimisha jamii juu ya shughuli za Afisi kupitia Mfumo wa TEHAMA
- Kuimarisha ufanisi wa kiutendaji na maslahi ya Wafanyakazi wa Afisi

