IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI

Idara hii inahusika na utoaji wa huduma za uendeshaji na utumishi, kusimamia maslahi ya rasilimali watu, pamoja na kutunza, kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu za Afisi

Idara ya Uendeshaji na Utumishi inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:

  1. Divisheni ya UendeshajiDivisheni hii inahusika na masuala ya utawala, uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila siku za Afisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
  2. Divisheni ya UtumishiDivisheni hii itahusika na masuala ya maendeleo na usimamizi wa rasilimali watu ndani Afisi ikiwemo ajira, mishahara, mafunzo kwa watumishi, upimaji utendaji kazi, upandishaji vyeo. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
  3. Divisheni ya Utunzaji KumbukumbuDivisheni hii itahusika na shughuli za uwekaji wa kumbukumbu na uhifadhi wa nyaraka na kazi mbali mbali za Afisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.