TAARIFA ZINAZOENDELEA KUSAMBAA MITANDAONI KUHUSIANA NA KUFANYIKA KWA USAILI WA FURSA ZA AJIRA ZA KAMPUNI YA INFINITY DEVELOPMENTS

OFISI YA RAIS

KAZI UCHUMI NA UWEKEZAJI

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ZINAZOENDELEA KUSAMBAA MITANDAONI KUHUSIANA NA KUFANYIKA KWA USAILI WA FURSA ZA AJIRA ZA KAMPUNI YA INFINITY DEVELOPMENTS KATIKA JENGO LA MAHAKAMA YA ZAMANI LILILOPO VUGA SIKU YA IJUMAA TAREHE 03/10/2025    

                                            

  1. Ofisi inawajulisha wananchi na waombaji wote walioomba na kujisajili kwa ajili ya  fursa za ajira katika Kampuni ya Infinity Developments, kwamba Taarifa zinazoendelea kusambaa Mitandaoni kuhusiana na kufanyika kwa usaili wa fursa hizo katika Jengo la Mahakama ya Zamani lililopo Vuga Siku ya Ijumaa tarehe 03/10/2025 SIO ZA KWELI.
  2. Ofisi itatoa Taarifa rasmi ya Mahali na Tarehe ya kufanyika kwa usaili huo.
  3. Ofisi inawakumbusha wananchi kujiepusha na kutoa, kupokea, kutuma au kusambaza taarifa wasizokuwa na uhakika nazo Mitandaoni.
  4. Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea Tovuti ya Ofisi www.orkuuzanzibar.go.tz kwa kubonyeza link iliyoandikwa “Taarifa Zinazoendelea Kusambaa Mitandaoni Kuhusiana Na Kufanyika Kwa Usaili Wa Fursa Za Ajira Za Kampuni Ya Infinity Developments” au piga simu nambari +255776914484.

  

    Imetolewa na:  

   KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO

      01/10/2025